Hukumu ya aliyeingia katika swawm ya kulipa kisha akataka kufungua

Swali: Ni lazima kukamilisha swawm ikiwa yule mfungaji analipa siku katika Ramadhaan kisha baadaye akapenda kula na badala yake kufunga siku nyingine?

Jibu: Kinachojulikana ni kwamba yule mwenye kuanza kufunga basi analazimika kukamilisha. Haifai kwake kula isipokuwa kwa sababu kama vile maradhi yaliyomtokea ghafla, safari au jambo jengine. Vinginevyo lililo la wajibu ni yeye kukamilisha swawm iliyofaradhishwa kama ya Ramadhaan au swawm ya nadhiri. Anatakiwa kuikamilisha na wala asifungue. Isipokuwa kwa sababu itayomruhusu kufungua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1247/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%B4%D8%B1%D8%B9-%D9%81%D9%8A-%D8%B5%D9%8A%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B6%D8%A7%D8%A1-%D8%AB%D9%85-%D8%A7%D8%B1%D8%A7%D8%AF-%D8%A7%D9%86-%D9%8A%D9%81%D8%B7%D8%B1
  • Imechapishwa: 10/05/2018