Swali: Ni njia ipi iliyotajwa katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):
وَإِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ
”… na hakika wale wasioiamini Aakhirah wanajitenga na njia hiyo.”[1]
Je, Hodhi itakuwa kabla ya Njia au baada yake? Je, Hodhi itakuwa kabla au baada ya kufanyiwa hesabu?
Jibu: Njia iliyotajwa katika Aayah kunakusudiwa njia ilionyooka. Imefasiriwa kama Uislamu, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan – na tafsiri zote hizo ni haki. Kinachokusudiwa ni njia ya Uislamu ambayo watu hawa wamepondoka kutokana nayo.
Hodhi itakuwa kabla ya Njia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu waliokuwa wananifuata watanijia katika Hodhi. Pale tu nitakapowaona, basi watakatwa kutokamana nami. Nitasema: “Ee Mola wangu! Maswahabah zangu! Maswahabah zangu!” Nidipo kusemwe: “Hakika wewe hujui waliyoyazua kabla yako.”[2]
Pia itakuwa kabla ya kufanyiwa hesabu. Hakuna baada ya Njia na Hesabu isipokuwa Pepo au Moto.
[1] 23:74
[2] al-Bukhaariy (6582) na Muslim (2304).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 313
- Imechapishwa: 19/05/2025
Swali: Ni njia ipi iliyotajwa katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):
وَإِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ
”… na hakika wale wasioiamini Aakhirah wanajitenga na njia hiyo.”[1]
Je, Hodhi itakuwa kabla ya Njia au baada yake? Je, Hodhi itakuwa kabla au baada ya kufanyiwa hesabu?
Jibu: Njia iliyotajwa katika Aayah kunakusudiwa njia ilionyooka. Imefasiriwa kama Uislamu, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan – na tafsiri zote hizo ni haki. Kinachokusudiwa ni njia ya Uislamu ambayo watu hawa wamepondoka kutokana nayo.
Hodhi itakuwa kabla ya Njia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu waliokuwa wananifuata watanijia katika Hodhi. Pale tu nitakapowaona, basi watakatwa kutokamana nami. Nitasema: “Ee Mola wangu! Maswahabah zangu! Maswahabah zangu!” Nidipo kusemwe: “Hakika wewe hujui waliyoyazua kabla yako.”[2]
Pia itakuwa kabla ya kufanyiwa hesabu. Hakuna baada ya Njia na Hesabu isipokuwa Pepo au Moto.
[1] 23:74
[2] al-Bukhaariy (6582) na Muslim (2304).
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 313
Imechapishwa: 19/05/2025
https://firqatunnajia.com/hodhi-ni-kabla-ya-njia/