Ninawauliza ndugu zetu: Je, sisi tunawaambia watu wanaokuja kwetu kujiandikisha kwetu ili baadaye wajiunge na jumuiya ya al-Hikmah au chama cha Iswlaah? Au watu wanakuja na kuondoka zao bila hata ya kuomba idhini? Hakika sisi tunakufunzeni kwa ajili ya Allaah na hatutaki kutoka kwenu malipo wala shukurani.
Hatutaki mfanye uasi wala mapinduzi pamoja nasi. Bali tunachotaka ni nyinyi kufahamu dini ya Allaah. Sisi tunaona kuwa inatuwajibikia kufunza – na sisi tunafanya kile ambacho Allaah ametuamrisha. Kwa ajili hiyo nawaambia:
مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ
“Kufeni kwa chuki zenu!”[1]
Tunamshukuru Allaah kuona vijana wanachukia mambo ya vyamavyama na kauli mbiu nyingine zote kabla ya Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mambo yote ya kipindi kabla ya kuja Uislamu nayaweka chini ya miguu yangu.”[2]
Kauli mbiu zote hizi zinatokana na kabla ya kuja Uislamu, ni mamoja vyamavyama hivo zimejficha au viko dhahiri.
Miongoni mwa mambo ya ajabu ni kuwasikia al-Ikhwaan al-Muslimuun wakisema kuwa wao sio chama. Nawaomba waende kwa wale wahusika wa vyama na wawaambie hivo. Je, wanataka kutucheka usoni mwetu? Nendeni katika jumuiya ya Hikmah uone itakuaje ukiwataka wakuozeshe, wakuchimbie visima na wakuchukulie kuwa ni ndugu zao bila kuomba uanachama nao au kujiunga nao. Wanachokonoa watu bongo, walisababisha kundi katika ndugu zetu kufukuzwa hapa. Hata hivyo, ndugu zetu wanajua kwamba hakuna walichotaka isipokuwa tu kuwanyima kheri. Karibu kila mtu ambaye alifukuzwa kwa sababu yao alirudi. Hakuna waliobaki isipokuwa tu wale wasioweza kusubiri hali ya wanafunzi.
Kwa hivyo nakushauri, ee mwanafunzi, usihatarishe maisha yako ambapo wakati fulani uko na al-Ikhwaan al-Muslimuun, wakati mwingine na jumuiya ya Hikmah na wakati mwingine na watafunaji miraa. Kwani hakika wewe utaulizwa juu ya maisha yako.
[1] 3:119
[2] Muslim (1218).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 346-347
- Imechapishwa: 11/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket