Swali: Ni ipi njia iliyowekwa katika Shari´ah ya kupangusa juu ya soksi?

Jibu: Ni kama kupangusa juu ya soksi za ngozi; ailowe mikono yake kwa maji kisha aweke vidole vya mkono wa kulia juu ya mguu wa kulia na vidole vya mkono wa kushoto juu ya mguu wa kushoto. Halafu avivute mpaka kwenye fundo za mguu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2016