Hivi ndio bora katika kutoa salamu

Swali: Maneno ya Malaika kumwambia Ibraahiym (´alayhis-Salaam):

قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ

”Wakasema: ”Amani.” Akasema: ”Amani.” (11:69)

Je, hapa inafahamisha kuwa bora ni kusema “Salaam” pasi na Alif na Laam?

Jibu: Hapana. Bora kwa mujibu wa Hadiyth Swahiyh, ni kama alivosema Allaah:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (04:86)

Sema:

السلام عليكم

“Amani iwe juu yenu.”

وعليكم السلام

“Nanyi amani iwe juu yenu.”

Hivi ndio bora. Lakini akisema:

سلام عليكم

“Amani iwe juu yenu.”

hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23380/حكم-القاء-السلام-بلفظ-سلام-عليكم
  • Imechapishwa: 07/01/2024