Swali: Kuna mtu siku zote kichwa chamuuma. Akaenda kwa tabibu ambaye alimpa kipande cha kitambaa kilichoshonwa na akamwambia akiweke chini ya kichwa chake wakati wa kulala. Pindi alipomuuliza kina nini, akamwambia kuwa kina Aayah za Qur-aan na du´aa za kinabii. Imewekwa katika Shari´ah kukitumia?

Jibu: Hapana. Hii ni hirizi. Kabla ya kwenda kulala asome Qur-aan na Suurah “al-Ikhlaasw”, “al-Falaq” na “an-Naas” na Aayah al-Kursiy. Haya ndio yenye kumnufaisha. Kuweka hirizi karibu na kichwa chake haijuzu na wala haimnufaishi kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (36) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2030%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 01/10/2020