Swali: Ni ipi daraja ya Hadiyth isemayo:
”Anayeswali Fajr msikitini, akabakia humo mpaka jua likapaa kiasi cha mkuki, basi atapata ujira wa Hijjah na ´Umrah.”?
Jibu: Hii imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini ninavyokumbuka katika cheni ya wapokezi kuna maneno. Haijulikani kuwa ni yenye usahihi madhubuti. Nilishawahi kuwakalifisha muda mrefu uliopita baadhi ya wanafunzi wetu wakusanye njia zake na kufuatilia katika sehemu zake, na mpaka sasa jambo hilo halijakamilika. Huenda nikalifanya mwenyewe na litakuwa hilo kwa idhini ya Allaah katika ijumaa nyingine.
Ama kilicho thabiti na kilichohifadhiwa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposwali Fajr hukaa mahali pake pa kuswali mpaka jua lichomoze. Akiswali humuomba Allaah na humtaja Allaah (´Azza wa Jall). Hili ni thabiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile imethibiti kutoka katika Hadiyth ya ´Amr bin ´Abasah katazo la kuswali baada ya Fajr mpaka jua lichomoze. Linapopinduka ndio aswali, kwani swalah inahudhuriwa na kushuhudiwa. Hii inafahamisha kuwa imesuniwa kuswali baada ya jua kuchomoza na kupondoka ndani ya msikiti. Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mtu kuswali kabla ya kutoka baada ya jua kupondoka. Vivyo hivyo nyumbani kwake swalah ya Dhuhaa. Ikiwa swalah baada ya kupondoka kwa jua hadi wakati wa joto kali itakuwa bora zaidi, kwani swalah ya Awwaabiyn ni pale joto la Dhuhaa linapoiva, pale ndama wanapopata joto la ardhi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1036/ما-صحة-حديث-من-صلى-الفجر-في-المسجد
- Imechapishwa: 19/01/2026
Swali: Ni ipi daraja ya Hadiyth isemayo:
”Anayeswali Fajr msikitini, akabakia humo mpaka jua likapaa kiasi cha mkuki, basi atapata ujira wa Hijjah na ´Umrah.”?
Jibu: Hii imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini ninavyokumbuka katika cheni ya wapokezi kuna maneno. Haijulikani kuwa ni yenye usahihi madhubuti. Nilishawahi kuwakalifisha muda mrefu uliopita baadhi ya wanafunzi wetu wakusanye njia zake na kufuatilia katika sehemu zake, na mpaka sasa jambo hilo halijakamilika. Huenda nikalifanya mwenyewe na litakuwa hilo kwa idhini ya Allaah katika ijumaa nyingine.
Ama kilicho thabiti na kilichohifadhiwa ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposwali Fajr hukaa mahali pake pa kuswali mpaka jua lichomoze. Akiswali humuomba Allaah na humtaja Allaah (´Azza wa Jall). Hili ni thabiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile imethibiti kutoka katika Hadiyth ya ´Amr bin ´Abasah katazo la kuswali baada ya Fajr mpaka jua lichomoze. Linapopinduka ndio aswali, kwani swalah inahudhuriwa na kushuhudiwa. Hii inafahamisha kuwa imesuniwa kuswali baada ya jua kuchomoza na kupondoka ndani ya msikiti. Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mtu kuswali kabla ya kutoka baada ya jua kupondoka. Vivyo hivyo nyumbani kwake swalah ya Dhuhaa. Ikiwa swalah baada ya kupondoka kwa jua hadi wakati wa joto kali itakuwa bora zaidi, kwani swalah ya Awwaabiyn ni pale joto la Dhuhaa linapoiva, pale ndama wanapopata joto la ardhi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1036/ما-صحة-حديث-من-صلى-الفجر-في-المسجد
Imechapishwa: 19/01/2026
https://firqatunnajia.com/hiki-ndicho-kilichothibiti-baada-ya-kuswali-fajr/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket