Hijrah kutoka miji ya Kiislamu ambapo wanaabudia makaburi

Swali: Katika baadhi ya miji ya Kiislamu kuna makaburi na yanafanyiwa Twawaaf. Je, ni wajibu kwa waislamu walioko huko kufanya Hijrah?

Jibu: Ni juu yako kufanya lile unaloweza. Ni juu yako kuwalingania na kuwabainishia. Ikiwa una elimu wabainishie kuwa ni Shirki na kwamba haijuzu kwa dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Ikiwa huna elimu waelekeze kwa wanachuoni ambao wanaweza kuwabainishia na kuwaelekeza. Fanya lile unaloweza. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=11649
  • Imechapishwa: 01/05/2015