Hijjah ya ambaye baadaye karitadi

Swali: Mtu alihiji kisha akaritadi – je, itamlazimu kuhiji tena?

Jibu: Hapana, hailazimiki. Akihidiwa na Allaah na akarudi katika Uislamu, hijjah yake ya awali hubakia sahihi.

Swali: Ni ipi tafsiri ya Aayah:

وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا

“Wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya kwishausokota ukawa mgumu.”? (an-Nahl 16:92)

Jibu: Maana aliyoitaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni kueleza hali ya watu waliokuwa katika kheri kisha wakayavunja matendo yao kwa kuingia katika ukafiri. Matendo yao hubatilika kwa sababu ya kuritadi, kama yule aliyefumua uzi wake baada ya kuumaliza.

Swali: Vipi ikiwa mtu amehiji kwa kujionyesha na ilikuwa ni hijjah ya faradhi – je, italazimu kuirudia?

Jibu: Hijjah ya kujionyesha ni batili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31136/هل-يجب-الحج-على-من-حج-ثم-ارتد
  • Imechapishwa: 05/10/2025