Miongoni mwa amana ni ile inayokuwa kati ya mume na mke katika yale mambo maalum. Hakika watu walio na ngazi mbaya zaidi mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah ni mwanaume anayefanya jimaa na mke na mke wake anafanya jimaa na yeye kisha anazungumza yaliyopitika kati yao. Haijuzu kwa mtu kuzungumza yaliyopitika kati yake na mke wake.
Vijana wengi wapumbavu utaona wanaburudika katika vikao na wanataja hayo mambo ya kibinafsi. Mmoja anamwambia mwenzake yale aliyofanya na mke wake miongoni mwa mambo ambayo mke wake hapendelei ayajue yeyote. Vivyo hivyo kila mtu mwenye akili ilio salama hapendelei yeyote ajue yaliyopitika na mke wake.
Kwa hivyo ni wajibu kwetu kuhifadhi amana.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/464-465)
- Imechapishwa: 19/08/2025
Miongoni mwa amana ni ile inayokuwa kati ya mume na mke katika yale mambo maalum. Hakika watu walio na ngazi mbaya zaidi mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah ni mwanaume anayefanya jimaa na mke na mke wake anafanya jimaa na yeye kisha anazungumza yaliyopitika kati yao. Haijuzu kwa mtu kuzungumza yaliyopitika kati yake na mke wake.
Vijana wengi wapumbavu utaona wanaburudika katika vikao na wanataja hayo mambo ya kibinafsi. Mmoja anamwambia mwenzake yale aliyofanya na mke wake miongoni mwa mambo ambayo mke wake hapendelei ayajue yeyote. Vivyo hivyo kila mtu mwenye akili ilio salama hapendelei yeyote ajue yaliyopitika na mke wake.
Kwa hivyo ni wajibu kwetu kuhifadhi amana.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/464-465)
Imechapishwa: 19/08/2025
https://firqatunnajia.com/hii-ni-tabia-ya-vijana-wengi-wapumbavu/