Hii leo hakuna haja ya adhaana ya kwanza siku ya ijumaa?

Swali: Haiwezeni kusemwa kwamba haja ya adhaana ya kwanza siku ya ijumaa imeondoka kutokana na uwepo wa vipaza sauti?

Jibu: Hapana. Je, mtu apinge yale yaliyofanywa na Maswahabah? Kile walichokifanya Maswahabah kipo ndani yake kheri na baraka. Ni kwa ajili ya kuwakumbusha watu ili wajitayarishe kwa ajili ya ijumaa. Kwa sababu wakisikia adhaana ya kwanza, huanza kujiandaa; yule anayehitaji kuoga au kujiandaa na mambo yake.

Swali: Katika baadhi ya nchi, muadhini wa kwanza na wa pili wanaadhini tofauti ya chini ya dakika tano katika msikiti mmoja?

Jibu: Hapana, kilicho bora ni adhaana ya kwanza iwe mapema kidogo kabla ya jua kupinduka. kile kinachofanywa katika msikiti wa Makkah, wa Madiynah na baadhi ya maeneo kingine si kizuri, kwani hakifikii lengo lililokusudiwa. Bora zaidi ni kwamba adhaana ya kwanza iwe mapema kidogo kabla ya jua kupinduka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31558/هل-تكفي-المكبرات-عن-الاذان-الاول-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 02/11/2025