Hayawezi kupingwa makatazo ya Mtume kuyatembelea makaburi kwa kitendo cha ´Aaishah

Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kulitembelea kaburi? Kwa sababu kuna dalili inayosema kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimtembelea ndugu yake ´Abdur-Rahmaan makaburini. Hadiyth hii ni nzuri na imepokelewa na an-Nasaa´iy. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Mosi: Tunatakiwa kutambua kwamba hatuwezi kukinzana maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya mwengine. Haijalishi kitu huyo mwengine ni nani. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ

“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi anapohukumu Allaah na Mtume Wake jambo lolote iwe wana chaguo katika jambo lao. “[1]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni (njia) bora na matokeo mazuri zaidi.”[2]

Hayawezi kupingwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi mara nyingi.”

kutokana na yale aliyoyafanya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

Kwanza ni kwa sababu kitendo chake kinaweza kuingiliwa na ima kupatia au kukosea. Hivo ni tofauti na maneno ya aliyekingwa na kukosea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Pili huenda alifanya hivo kwa kusahau ikiwa alifikiwa na Hadiyth, akaifasiri vyengine na mfano wa hayo.

Lakini kuna Hadiyth katika “as-Swahiyh” ya Muslim wakati ´Aaishah alipopoteana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamkuta ametembelea al-Baqiy´ ambapo akamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Unaona niseme vipi?” Akamfunza namna atavyoyasalimia makaburi. Lakini kitendo hichi pia hakipingani na matembezi. Kwa sababu tunasema hapana neno endapo mwanamke atapita makaburini ambapo akasimama na kuwaombea du´aa waliyomo kwenye makaburi. Ama yeye kutoka nyumbani kwake kwa ajili ya kwenda kuyatembelea makaburi ni kitendo cha haramu.

[1] 33:36

[2] 04:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1637
  • Imechapishwa: 10/05/2020