Swali: Nini maoni yenu kuhusu mwanaume kuwa na haya nyingi sana na anaweza kujikuta katika matatizo yaliyo juu ya uwezo wake na yanaweza kumsababishia matatizo na huzuni kwa muda mrefu wa maisha yake au maisha yake yote?
Jibu: Ni lazima kuwe na haya, ni kitu kisichoenda kinyume na Shari´ah. Haya isiyoamrisha mema, haikatazi maovu na wala haifanyi wajibu: haizingatiwi kuwa haya, hii ni woga, udhaifu na kushindwa. Ni lazima kuwe na haya inayolingana na Shari´ah. Maana ya haya hiyo ni ile inamzuia na maadili mabaya na inamsaidia katika maadili mazuri, hii ndiyo haya ya Kishari´ah. Lakini haya inayomzuia na mambo ya wajibu, kutotangamana na watu wema, kutafuta elimu au yanayofanana na hayo, basi hii si haya, hii ni udhaifu na uvivu.
Swali: Ninamaanisha haya inayomzuia na mema – mema ya dini – lakini haya ambayo inaweza kumfanya mtu akawa na haya kiasi cha kujikuta katika huduma, mialiko au ndoa?
Jibu: Afundishwe na apewe nasaha. Ikiwa kuna khofu juu yake, basi anasihiwe.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25202/ما-ضابط-الحياء-المحمود-في-الرجل
- Imechapishwa: 17/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)