Miongoni mwa maovu yanayofanyika [katika minasaba ya ndoa] ni kwamba baadhi ya wanawake wanakuja na vifaa vya picha na wanawachukua picha walioko pale. Huenda baadhi ya wanaume wapumbavu wakafanya hivo kwa kujificha. Haya pia ni maovu makubwa…

Baya zaidi kuliko hilo ni kwamba baadhi ya watu wanakuja na video camera na wakawachukua video walioko pale. Haya yote yamekuja kutokea kipindi cha nyuma.

Kwa kufupisha ni kwamba kuhudhuria karama ya ndoa ni Sunnah. Lakini kama kutakuwa kuna mambo ya haramu, kama utaweza kuyazuia hivyo hudhuria. Usipoweza usihudhurie.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1459