Swali: Tuna mlinganizi mmoja anayesema kuwa Salaf waliigawanya Tawhiyd katika mafungu mawili; Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah tu, kisha baadae wakalazimika kuzidisha kigawanyo cha tatu; Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat kwa sababu ya kukabiliana na mapote potevu. Kujengea juu ya hili yeye anampa udhuru mwenye kuongeza Tawhiyd-ul-Haakimiyyah kwa sababu bado lengo ni kutaka kuweka mambo wazi na kubainisha.
Jibu: Haya ndio makusudio yake. Makusudio yake ni kutaka kutakasa Tawhiyd-ul-Haakimiyyah. Sentesi ya maneno yake ya kwanza ni mazuri.
Ni kweli ya kwamba Tawhiyd kwa njia ya ujumla ni aina mbili:
1- Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.
2- Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.
Kuhusiana na Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat inaingia katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hili ni kwa njia ya ujumla.
Upambanuzi huu lengo ni kama walivyosema Salaf; kuna mapote yamejitokeza ambayo yanapinga Allaah kuwa na majina na sifa au wanayawekea Ta´wiyl. Hivyo ndio maana wakawa wamepambanua Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat kwa kuitoa katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Vinginevyo inaingia humo. Lengo la kuipambanua ni kutaka kuwaraddi wale wenye kuyaharibu majina na sifa za Allaah.
Tawhiyd-ul-Haakimiyyah. Hii hatuijui. Isitoshe haipatikani katika vitabu vyote vya ´Aqiydah. Hakuna Tawhiyd-ul-Haakimiyyah. Haakimiyyah inaingia katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah pia. Hakuna haja ya kuipambanua.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Imechapishwa: 04/04/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)