Hata kama wameshazaa watoto mia moja

Swali: Mwanamme mmoja amemtaliki mke wake mara tatu katika nyakati mbalimbali: mara ya kwanza ilikuwa Sanaa, mara ya pili Taiz na mara ya tatu Bayda. Wameshazaa watoto saba. Walimuuliza ´Umar bin Haafidhw Bayda ambaye akawajibu kuwa jambo ni lenye sura tofauti kutokana na kwamba wameshazaa watoto saba. Unasemaje juu ya fatwa hiyo?

Jibu: Ikiwa alimwacha baada ya yeye kumrejea, anaharamika kwake mpaka aolewe na mume mwingine. Na ikiwa alimwacha  kabla ya kumrejea, basi ile talaka ya pili na ya tatu haikupita. Katika hali hiyo iliyopita ni ile talaka moja peke yake.

Kuhusiana na maneno ya masikini huyu kwamba wameshazaa naye watoto saba, talaka ni yenye kupita hata kama watakuwa na watoto mia moja. Na ikiwa haikupita, basi asitilie manani jambo hilo. Yeye ndiye anayejua zaidi kama alimtaliki kisha akamrejea, akamtaliki kisha akamrejea, akamtaliki kisha akamrejea. Katika katika hali hizo zimepita na haruhusu kumuoa mpaka aolewe na mume mwingine. Na ikiwa alimwacha mahali fulani kisha akahamia mahali pengine pasi na kumrejea, kisha akahamia mahali pengine na akahamia kwa mara ya tatu mahali pengine, katika hali hiyo imepita tu talaka moja. Zile talaka mbili zingine hazikupita.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 413-414
  • Imechapishwa: 09/07/2025