Swali: Ipi hukumu ya kuhudhuria mwanamke katika hafla za ndoa ambazo zina wanawake walio uchi?
Jibu: Hili ni munkari. Na hili limeenea sana leo katika mikusanyiko ya wanawake – sehemu za starehe, minasaba ya ndoa hususan wajane wanahudhuria na nguo mbaya, mpaka walio uchi wanahudhuria – A´udhubillaah. Na hakuna yeyote anaekataza; si walii wake, mama yake wala yeyote wala waliohudhuria. Bali wanafurahishwa na hilo. Huu ni munkari na khatari kubwa kwa Ummah. Na hili likitokea katika mikutano baina ya wanawake, yule ambaye anaweza kubadili hili anaweza kukataza wanawake, ni wajibu kwake kuhudhuria kwa ajili ya kukataza munkari. Ama yule asiyeweza hilo [kukataza munkari] haijuzu kwake kuhudhuria kwa kuwa asipate madhambi akawa ameshiriki. Kwa kuwa mwenye kuacha kukataza munkari naye anaweza hilo anakuwa ameshiriki kwa yaliyofanya. Usihudhurie.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/allmohadrat?page=4
- Imechapishwa: 09/11/2014
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Inafaa kusikiliza nyimbo za wanawake siku ya harusi?
Swali: Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amewajuzishia wanaume kusikiliza nyimbo za wanawake wanapopiga dufu? Jibu: Hili wamelijuzisha wanachuoni wengi katika mnasaba wa ndoa tu [wanawake kuimba]. Katika mnasaba wa ndoa wanawake wanaimba wao kwa wao nyimbo zenye kujulikana ambazo hazina mdundiko, muziki na ala za muziki. Jambo lingine…
In "Harusi"
Wanawake kunyanyua sauti zao katika nyukumbi za harusi
Swali: Una nini cha kuwaambia wale wamiliki wa nyukumbi za starehe na nyukumbi za harusi kutokana na yale yanayopatikana katika kunyanyua sauti za nyimbo kupitia vipaza sauti au wanakaa wanaume wanasikiliza nyimbo za watoto wa kike inayotoka kwa nje. Unasemaje juu ya hilo? Jibu: Maoni yangu ni kwamba kitendo hichi…
In "Mchanganyiko kati ya jinsia mbili"
Kuhudhuria sherehe za harusi mahali kuna maovu ambayo mtu hatoyashiriki
Swali: Sherehe zetu nyingi huwa hazina mambo ya maovu isipokuwa tu wakati wanaume wanaingia kwenye ukumbi wa chakula ulio karibu na ukumbi wa wanawake ndipo wanaweza kusikia sauti za wanawake kwa jina “vigelegele”. Je, kitendo hichi ni maovu? Katika hali hii ni wajibu kwetu kutoka nje baada ya kuhudhuria katika…
In "Mfumo wa Da´wah na ya kipaumbele"