Swali: Je, kufanya haraka wakati wa swalah kunapunguza thawabu?

Jibu: Kufanya haraka kunachukiza. Sunnah ni kutofanya haraka wakati wa kutembea, azifanye karibu hatua zake, azingatie kuwa ametoka kwa ajili ya ´ibaadah na jambo kubwa na kwamba kwa kila hatua moja anaandikiwa thawabu na anafutiwa dhambi. Hivyo anakosa baadhi ya thawabu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25223/هل-العجلة-في-السعي-للصلاة-تنقص-من-اجرها
  • Imechapishwa: 19/02/2025