Swali: Vipi tutaamiliane na mtu ambaye ana ushabiki kwa walinganizi wapotevu na vipi tutaenda daraja kwa daraja katika kumnasihi, lini anasuswa na vipi inakuwa kuwasusa?

Jibu: Leo kila mtu anasema kuwa fulani ni mpotevu na ni mzushi. Kumekuwa hakuna kigezo chenye kujulikana.

Lakini hata hivyo ikithibiti kuwa ni walinganizi wapotevu kinachotakiwa ni kuwanasihi na kuwapa mawaidha. Wakiitikia, ni vizuri, na wasipoitikia mtu ametekeza dhimma kwao. Baada ya hapo inatakiwa kuwasusa na kujitenga nao mbali. Jengine inatakiwa kutahadharisha nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 28/06/2020