Nitakutajia baadhi ya alama za Hizbiyyuun ili usitoke kwenye chama kimoja ukaingia katika chama kingine. Hizbiy kuja kwako na kukwambia kuwa yuko tayari kukusaidia – lakini kwa sharti ujiunge nao.
Anaweza kuja kwako na kukwambia kuwa yuko tayari kukufungulia masomo ya kuhifadhi Qur-aan – lakini kwa sharti wanafunzi wajiunge nao.
Anaweza kuja kwako na akakwambia kuwa yuko tayari kukufungulia kituo, lakini akiona kuna mwanafunzi ambaye ana uwezo wa kuendesha kituo hicho, anampa hati ya mwisho: ama ujiandikishe nasi au tufanye mtu mwingine ndiye awe mkuu.
Pengine wasiseme chochote katika hayo. Hivi sasa wako na masomo ya kuhifadhi Qur-aan, vituo na jumuiya kwa ajili ya manufaa ya vyama vyao. Hamtosubiri? Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ
”… na Tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoa watu kwa amri Yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na ishara zetu.”[1]
Hakusema kuwa aliwafanya viongozi katika wao kutokana na pesa zao. Hamuwezi kuzishinda nafsi zenu wala jamii isipokuwa kwa kusubiri. Mtu akikujieni na kukuombeni kuwapa kiapo cha usikivu na kuwaahidini kukusaidieni, kubalini msaada ikiwa haukufungamana na masharti yoyote. Sisi hatuuzi ulingano wetu. Hatuziuzi nafsi zetu kwa ajili ya dhahabu na fedha.
[1] 32:24
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 355
- Imechapishwa: 29/06/2025
Nitakutajia baadhi ya alama za Hizbiyyuun ili usitoke kwenye chama kimoja ukaingia katika chama kingine. Hizbiy kuja kwako na kukwambia kuwa yuko tayari kukusaidia – lakini kwa sharti ujiunge nao.
Anaweza kuja kwako na kukwambia kuwa yuko tayari kukufungulia masomo ya kuhifadhi Qur-aan – lakini kwa sharti wanafunzi wajiunge nao.
Anaweza kuja kwako na akakwambia kuwa yuko tayari kukufungulia kituo, lakini akiona kuna mwanafunzi ambaye ana uwezo wa kuendesha kituo hicho, anampa hati ya mwisho: ama ujiandikishe nasi au tufanye mtu mwingine ndiye awe mkuu.
Pengine wasiseme chochote katika hayo. Hivi sasa wako na masomo ya kuhifadhi Qur-aan, vituo na jumuiya kwa ajili ya manufaa ya vyama vyao. Hamtosubiri? Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ
”… na Tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoa watu kwa amri Yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na ishara zetu.”[1]
Hakusema kuwa aliwafanya viongozi katika wao kutokana na pesa zao. Hamuwezi kuzishinda nafsi zenu wala jamii isipokuwa kwa kusubiri. Mtu akikujieni na kukuombeni kuwapa kiapo cha usikivu na kuwaahidini kukusaidieni, kubalini msaada ikiwa haukufungamana na masharti yoyote. Sisi hatuuzi ulingano wetu. Hatuziuzi nafsi zetu kwa ajili ya dhahabu na fedha.
[1] 32:24
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 355
Imechapishwa: 29/06/2025
https://firqatunnajia.com/hapo-ndipo-hizbiyyuun-watakusaidia/