Swali: Ni yepi yaliyopokelewa katika Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya suala la kufaa mume kumpiga mwanamke?

Jibu: Sijui isipokuwa yale yaliyotajwa ndani ya Qur-aan. Qur-aan imetaja dalili juu ya hilo:

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ

“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.” (04:34)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wanayo haki wanawake juu yenu ya kuwapa matumizi na kuwavisha kwa wema. Mnayo haki wanamme juu yao wasimwache kukanyaga kitanda chenu yule mnayemchukia na wasimpe idhini ya kuingia katika nyumba zenu yule mnayemchukia. Wakifanya hivo, basi wapigeni kipigo kisichoumiza.”

Bi maana msiwapige kipigo kizito. Inahusiana na kipigo cha kuwatia adabu. Isiwe kipigo cha khatari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21660/ما-الذي-جاء-في-السنة-بشان-ضرب-المراة
  • Imechapishwa: 05/09/2022