Hapa ndipo mtu analipwa kutokana na nia yake

Swali: Ni kwa nini anaandikiwa dhambi ambaye amenuia kufanya dhambi lakini asiifanye?

Jibu: Iwapo atajitahidi kuifanya na akafanya akiwezacho, lakini akazuiwa kati yake yeye na dhambi hiyo. Mfano wa mtu ambaye ametaka kumuua rafiki yake, mfano mwingine mtu ambaye amevunja nyumba na kuingia ndani na alipotaka kuiba akazuiwa baina yake yeye na jambo hilo. Mifano ni mingi mfano wa hiyo. Kwa ajili hiyo ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Muuaji na muuliwaji wote wawili Motoni.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24349/هل-تكتب-السيىة-على-من-هم-بها-ولم-يعملها
  • Imechapishwa: 02/10/2024