Hapa ndipo mlezi atalazimika kumwamrisha mtoto kuswali

Swali: Je, mtoto wa miaka saba anayetakiwa kuamrishwa swalah afanyiwe ukali au aamrishwe tu?

Jibu: Ni lazima kwa mlezi wake kumwamrisha kuswali. Ni lazima kwa msimamizi wake kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Waamrisheni… ”

Msingi wa amri ni uwajibu.

“… na wapigeni kwayo pindi wana miaka kumi… ”[1]

Lengo ni ili azowee kheri. Baadhi ya watoto wanaweza kubaleghe kabla ya miaka 10, wengine 11 na wengine 12.

[1] Abu Daawuud (495). Hadiyth ni Swahiyh. Tazama ”Nasb-ur-Raayah” (1/298) kwa tamko kama hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23973/هل-امر-الابناء-بالصلاة-لسبع-على-الوجوب
  • Imechapishwa: 08/08/2024