Swali: Je, uchaguzi na kupiga kura si ni kujenga urafiki na makafiri na kuwatawala kwao waislamu?

Jibu: Je, uongozi utaanguka na nchi itabaki bila raisi endapo waislamu hawatomchagua yeyote katika nchi hii? Au litatimia jambo la uraisi kwa hali yoyote? Ikiwa waislamu watamchagua mtu ambaye wanaamini kuwa atawanufaisha waislamu, au wakiacha kupiga kura basi kuna uwezekano utawala ukaenda kwa mtu ambaye wanamfikiria vibaya, basi katika hali hiyo italazimika kwao kupiga kura. Ikiwa wana dhana kubwa kuwa mgombea fulani atawapendelea waislamu zaidi kuliko mwengine na kwamba wakiacha kumpigia kura basi hilo litapelekea manyanyaso zaidi kwa waislamu, basi watasaidiwa watu wasiofanya uadilifu juu ya haki za waislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.salafi-dawah.com/uploads/1/5/0/0/15007852/shaykh_al-luhaydaan_-_wouldnt_voting_or_participating_in_elections_be_considered_as_assisting_the_kuffaar_in_having_authority_over_the_muslims.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2022