Hapa ndipo inapendeza kumuoa mwanamke asiyekuwa na mama

Swali: Katika ”Zaad-ul-Mustaqni´” kumependekezwa kumuoa msichana bikira na asiyekuwa na mama. Ni yepi makusudio?

Jibu: Kwa sababu mama hukuharibia msichana wako. Lakini si sahihi. Sio mama wote huwaharibu wasichana zao. Lakini ikiwa mama anatambulika kusababisha matatizo na mfano wake, basi asimuoe msichana wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 19/07/2024