Swali: Ni ipi hukumu ya kuchelewesha adhaana baada ya kuingia wakati wake?
Jibu: Ikiwa mtu yuko ndani ya mji, basi hatakiwi kuchelewesha kuanzia wakati wake wa mwanzo. Kwa sababu hilo linapelekea katika vurugu, kutofautiana kwa waadhini na watu wakaanza kuchanganyikiwa ni nani kati ya waadhini hao ambaye amepatia. Lakini mtu akiwa nje ya mji, wana khiyari. Hata hivyo bora ni kuadhini pale tu unapoingia wakati wake na waswali. Kwa sababu kutanguliza swalah mwanzoni mwa wakati wake ndio bora, muda wa kuwa haikuwekwa katika Shari´ah kuichelewesha; katika hali hiyo itacheleweshwa. Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
Tulikuwa tumefuatana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) safarini. Muadhini akasimama ili aadhini kwa ajili ya swalah ya Dhuhr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Acha kupoe.” Kisha akataka tena kuadhini ambapo akasmea: “Acha kupoe.” Kisha akataka tena kuadhini ambapo akasmea: “Acha kupoe.” Mpaka vivuli vikawa sawa kwa urefu ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika ukali wa joto unatokana na ghadhabu ya Moto.”[1]
Haya yanafahamisha kuwa adhaana imewekwa katika Shari´ah pale unapoingia wakati wa kuswali. Ikiwa swalah inaswaliwa pale tu kunapoingia wakati wake, basi kunaadhiniwa pale tu muda wake unapoingia, na ikiwa swalah inatakiwa kucheleweshwa, kama vile swalah ya Dhuhr wakati jua linapokuwa kali na swalah ya ´Ishaa, basi itacheleweshwa kuadhiniwa mpaka wakati wa kuswaliwa – muda wa kuwa sio katika miji na vijiji vilivyo na waadhini. Vinginevo haitakikani kwa mtu kuchelewesha ule muda ambao watu wanaadhini.
[1] al-Bukhaariy (629) na Muslim (616).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/189-190)
- Imechapishwa: 03/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/189-190)
Imechapishwa: 03/04/2026
https://firqatunnajia.com/hapa-ndipo-inafaa-kuchelewesha-adhaana/