Hapa ndipo anaswaliwa aliyekufa mji mwingine

Swali: Ni jambo linalotambulika kuwa misikiti yote ya Hadhwramawt wanamswalia swalah ya jeneza maiti aliyekufa mji mwingine na tumewasikia wengine wakisema kuwa ni Bid´ah. Tunaraji utatubainishia dalili za pande mbili.

Jibu: Maiti asiyekuwepo ikiwa hakuswali katika mji wake ni sawa kumswalia katika uwanja. Vivyo hivyo ni sawa endapo ataswaliwa msikitini. Hata hivyo watu wanaomswalia wanatakiwa kuwa wengi, jambo ambalo linapatikana uwanjani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia an-Najaashiy katika uwanja.

Lakini kama mtu ameswaliwa katika mji wake, itambulike kuwa kuna Maswahabah wengi waliokufa mbali na miji yao na haikuthbiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalia.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 350
  • Imechapishwa: 05/05/2025