Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuporomosha mimba kabla kipomoko hakijaumbwa?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa inafaa inafaa kuporomosha tone la manii kabla haijatimiza siku arobaini kwa kutumia madawa yanayofaa kwa sharti mimba hiyo iwe bado ni tone la manii. Ama ikishapiga hatua kutoka tone la manii kwenda kipande cha damu na kutoka kipande cha damu kwenda kinofu cha nyama, basi udhahiri wa maneno ya wanachuoni ni kwamba haijuzu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 12/06/2020