Hali tatu ambapo imamu amesahau kukaa Tashahhud ya kwanza

Swali: Imamu alisahau kukaa katika Tashahhud ya kwanza na badala yake akasimama. Aliposimama na akanyooka maamuma wakasema “Subhaan Allaah” ambapo imamu akarudi kukaa. Ni kipi wanachotakiwa kufanya maamuma ikiwa ni haramu kwa imamu kurudi kukaa baada ya kuwa amekwishasimama? Je, wamfuate?

Jibu: Ndio, wamfuate. Kuna hali tatu kwa imamu:

1- Akakumbuka au akakumbushwa kabla ya kusimama sawasawa. Katika hali hii ni lazima arudi.

2-  Akakumbuka baada ya kuwa amekwishasimama sawasawa. Huyu imechukizwa kwake kurudi. Lakini hakuna neno iwapo atarudi.

3- Akawa ameshaanza kusoma al-Faatihah. Katika hali hii imeharamishwa kurudi. Haiharamiki kwake isipokuwa pale atakapoanza kisomo. Akianza kusoma al-Faatihah basi itakuwa ni haramu kwake kurudi. Ama akisimama sawasawa na akawa hajaanza kusoma al-Faatihah, hapa imechukizwa kurudi. Akirudi ni sawa lakini hata hivyo imechukizwa. Lakini akiwa hajasimama sawasawa hapa ni lazima kwake kurudi. Katika hali zote hizi anatakiwa kusujudu sijda ya kusahau.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 31/05/2019