Hakuwahi kusoma katika swalah kwa sababu hakumsikia imamu

Swali: Kuna mtu alijiunga na imamu katika Rakaa´ ya kwanza. Wakati imamu alipokaa katika Tashahhud ya kwanza akakaa naye. Pindi imamu aliposimama katika Rakaa´ ya tatu maamuma huyu hakumsikia isipokuwa mpaka baada alipokuwa amefika katika Rukuu´. Hivyo akawa amesimama moja kwa moja na akaenda naye katika Rukuu´. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Kuchelewa kwake ni kwa sababu ya udhuru; hakumsikia imamu. Maadamu amewahi Rukuu´ hahitajii kusimama na kusoma kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020