Hakuna uongo mweupe wala hakuna uongo wa april katika Uislamu

Miongoni mwa vitu vinavyohusiana na vyombo vya khabari vya uwongo ni yale yaliyosimuliwa na Jundub bin Jundub (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa ameota kuhusu bwana mmoja aliyekuwa anaadhibiwa kwa ndoano inayoendeshwa kwenye kona moja ya mdomo, jicho na pua na kisha kuvutwa kutoka nyuma hadi kona nyingine ya mdomo, jicho jingine na pua nyingine. Wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipouliza kuhusu bwana huyo, akapewa khabari kwamba ni mtu ambaye alikuwa akisema uwongo mpaka unafika kwa umati wa watu. Dini haina kitu kinachoitwa uwongo mweupe wala uwongo mweusi. Uislamu hauna kitu kinachoitwa uwongo wa april.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 184
  • Imechapishwa: 15/02/2025