Hakuna kizuzi kizito zaidi kuliko madai

Swali: Amesema:

“Hakuna njia ya kumfikia Allaah iliyo karibu zaidi kuliko ya ´ibaadah. Hakuna kizuizi kizito zaidi kuliko madai.”

Nini maana ya madai hayo?

Jibu: ´Ibaadah ni unyenyekevu mbele ya Allaah na kumtii. Madai ni mtu kujidai kwamba yeye ni hivi au vile, akajiona au kujisifia kwa matendo yake kuwa yeye ni mcha Allaah, anasimama usiku kwa swalah na anafunga sana. Matokeo yake akatahiniwa kujionyesha na kujiona ana fadhilah kwa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31128/ما-معنى-عبارة-لا-حجاب-اغلظ-من-الدعوى
  • Imechapishwa: 04/10/2025