Hakuna kikomo maalum cha wanandoa kuwa mbalimbali

Swali: Je, inajuzu kwa mume kuwa mbali na mkewe kwa zaidi ya miezi sita kwa sababu mume yuko Saudi Arabia na yeye mwanamke yuko Misri?

Jibu: Hili linategemea kutegemea na mazingira; anaweza kulazimika kuzidisha na kupunguza muda. Hakuna muda uliowekewa kikomo safarini. Imepokelewa ya kwamba ´Umar alikuwa akiwawekea muda wa miezi sita maaskari. Hata hivyo halina dalili ya wazi. Ninachokusudia ni kwamba mtu anaweza kuhitaji zaidi ya miezi sita katika kutafuta riziki na pengine ikamtosha miezi miwili na mitatu. Kwa vyovyote vile azingatie manufaa. Anatakiwa kumcha Allaah na kujitahidi. Kama anachelea juu ya mkewe basi asiwe mbali kwa miezi sita. Awe karibu nao na afanye kazi kwao katika mji wao, mwanamke asafiri pamoja naye au muda uwe chini ya miezi sita kama mfano wa miezi miwili au mitatu. Anapaswa kujitahidi kwa sababu yeye ndiye mjuzi zaidi wa nafsi yake, mkewe na khatari iliopo. Kwa hivyo asikomeke na miezi sita, miezi miwili wala miezi mitatu. Bali iwe kutegemea na mazingira yalivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24641/ما-الضابط-في-مدة-بعد-المغترب-عن-زوجته
  • Imechapishwa: 17/11/2024