Swali: Una lolote la kuwaambia Waislamu kutokana na fitina hizi ambazo haziko wazi zimewachanganya mpaka wamekuwa hawajui haki iko wapi?

Jibu: Haki iko wazi na himdi zote ni za Allaah. Kila Muislamu anajua ni wapi haki ipo, nayo ni kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kushikamana na Dini hii. Pasina kujali ni fitina kubwa na nyingi zitavokuwa, haki iko wazi na himdi zote ni za Allaah. Hakuna utatizi ndani yake. Uokozi juu ya fitina hizi ni kushikamana na Qur-aan na Sunnah na kushikamana na mkusanyiko wa Waislamu na kiongozi, kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyousia hilo wakati Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anhu) alipomuuliza kuhusu fitina wakati zitapokuwa nyingi na kubwa. Akamuuliza la kufanya wakati atapokumbana na hilo. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Shikamana na mkusanyiko wa Waislamu na kiongozi wao.”

Kwanza tunatakiwa kushikamana na Qur-aan na Sunnah, kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kushikamana na mkusanyiko wa Waislamu na kiongozi wa Waislamu na kuomba Du´aa sana. Muombe Allaah Akukinge na fitina hizi na Awaokoe Waislamu na shari yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/leqa10-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 13/12/2014