Haitoshi kupiga msitari kwenye picha

Swali: Ni ipi hukumu ya picha za viwiliwili bila ya kichwa?

Jibu: Kiondolewe kichwa, na si kupiga msitari tu kama wanavofanya baadhi ya watu.

Swali: Katika hali hiyo haiwi ni mchoro wa viumbe vyenye roho?

Jibu: Kukiondolewa kichwa kabisa kwa mfano wa kukikata. Kiondolewe kabisa na mtu awe kama kijimti.

Swali: Vipi kutenganisha kati ya kichwa na kiwiliwili?

Jibu: Haitoshi, hapana, haitoshi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24806/حكم-الصورة-المجسدة-دون-الراس
  • Imechapishwa: 14/12/2024