Salafiyyuun wote ulimwenguni wenye kuniuliza kuhusu kuanzisha jumuiya (taasisi), basi huwa nikiwaambia ya kwamba baada ya kudurusu mambo haya mimi naonelea kuwa haijuzu kuanzisha jumuiya hizi isipokuwa kwa dharurah. Madhara yake yanajulikana. Dharurah yenyewe ni kwa mfano watu wako katika mji ambapo hakuruhusiwi kufanya Da´wah isipokuwa iwe chini ya jumuiya fulani. Katika hali hii ndio itakuwa inajuzu, kwa dharurah, kwa sharti kusikuwepo nidhamu maalum za jumuiya hii. Mfumo wake uwe ni wa Salaf. Vilevile kusifungamanishwe kupenda na kuchukia kukawa ni kwa ajili ya jumuiya hii.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda “as-Salafiyyah wa Hayaatah” https://www.youtube.com/watch?v=Jq9DehxRLE8
  • Imechapishwa: 16/11/2014