Haijuzu kwa mwanaume kuwabusu Mahaarim wake?

Swali: Nimesikia kwamba haijuzu kwa mwanaume kumbusu yeyote miongoni Mahaarim wake isipokuwa mke wake, hata dada yake au msichana yake haruhusiwi kumbusu. Je, hilo ni sahihi?

Jibu: Hili halina msingi. Inajuzu kumbusu Mahaarim wake kama mama yake, shangazi yake na dada yake. Hakuna tatizo katika hilo. Lakini akimbusu dada yake au msichana wake, basi iwe shavuni, puani au kichwani. Hilo ndio bora zaidi. Ama busu mdomoni, kuliacha ndilo bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1465/حكم-تقبيل-المحارم
  • Imechapishwa: 20/12/2025