Haijuzu kuswali kwenye msikiti ulioambatana na kaburi

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye msikiti ulio na kaburi lakini kaburi hili haliko upande wa Qiblah? Inajuzu kuswali au swalah inakubalika pamoja na kuwa mtu anapata dhambi?

Jibu: Hapana, haijuzu kuswali kwenye msikiti ambao umejengwa kwenye kaburi ambalo limekamatana nao, sawa kaburi hilo likiwa kwa mbele, nyuma, kulia au kushoto. Maadamu kaburi limekamatana na msikiti haijuzu na haijalishi liko upande gani wa msikiti.

Lakini kaburi likiwa limetengana na msikiti kwa kuwepo barabara katikati hakuna neno. Kwa sababu kaburi limetengana na liko mbali na msikiti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2138
  • Imechapishwa: 12/07/2020