Swali: Unasemaje juu ya ISIS inayotajwa kwenye vyombo vya khabari?

Jibu: Ni jambo lisolokuwa na shaka ya kwamba kila kheri inapatikana katika yale yaliyokuja na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yakatendewa kazi na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Allaah (´Azza wa Jalla) Amemtuma Muhammad kuwa ni Rahmah kwa walimwengu:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ

Na Hatukukutuma isipokuwa (uwe) ni Rahmah kwa walimwengu.” (21:107)

Amemkamilishia Dini. Maswahabah walifahamu Dini ya Allaah sawa na wakaitendea kazi sahihi. Walijaza miji waliyofika ndani yake kheri na baraka. Watu wakaingia katika Uislamu makundi kwa makundi. Hali iliendelea kuwa hivyo mpaka wakati ambapo kulitokea watu ambao walifikiria kuwa wao wameifahamu Dini ya Allaah bora zaidi kuliko Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba wana hisia zenye nguvu juu ya Dini ya Allaah kuliko Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nao si wengine isipokuwa ni Khawaarij. Khawaarij hawa hudhihiri katika kila karne. Kila wakati wanapojitokeza wanakatika. Wote wana sifa ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizoelezea. Ni wadogo kiumri na ni wapumbavu wa akili. Wanazungumza kwa maneno bora zaidi ya viumbe. Wakati wanaposoma Qur-aan wanafikiria kuwa iko pamoja na wao wakati iko dhidi yao. Imani yao haivuki shingo zao. Wanawaua Waislamu na wanawaacha makafiri. Wanamkufurisha kila mwenye kwenda kinyume na wao. Yule anayeenda kinyume na wao ni kafiri kwa mujibu wao na hivyo wanaonelea kuwa damu yake ni halali. Wanaichukua mali yake na wanawake wake wanawafanya kuwa watumwa.

Mmoja wao alinambia siku moja wakati wa Hajj:

Je, unawaona mamilioni tatu hawa ya mahujaji? Hakuna yeyote anayemjua Allaah.”

Watangu wao walimkufurisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) kwa kuwa alipigana pasina kuchukua ngawira. Hizi ndio fikira zao. Hawa wanapatikana katika ISIS. Katika wao kuko watu wenye fikira zote za Khawaarij. Katika wao kuko watu wenye baadhi ya sifa za Khawaarij. Wote wanaenda kinyume na Sunnah, wanaudhuru Ummah na kuuvurugia Ummah Jihaad iliyowekwa katika Shari´ah. Wanazielekeza silaha zao dhidi ya Ahl-us-Sunnah kwa sababu wanaonelea kuwa ni wenye kuritadi na ni wanafiki. Wanaonelea kuwa kuwaua wao kwanza ni aula zaidi kabla ya mayahudi na manaswara.

Hivi katika Ramadhaan mayahudi wameivamia Ghaza na kuwaua Waislamu. Je, watu hawa ´Iraaq na Shaam wameenda Palestina kuwalinda Waislamu? Hapana. Badala yake wameenda kwenye mpaka wa Saudi Arabia – nchi ya Tawhiyd na Sunnah. Ilikuwa siku ya Ijumaa ya kwanza ya Ramadhaan. Ilikuwa wakati wa Swalah ya Ijumaa. Kwa kuwa wanajua kuwa jeshi la kisaudi linaswali Swalah ya Ijumaa. Wakalipua gari, wakaingia katika mji na kukusudia ufisadi, lakini Allaah Akawaua.

Ndugu zetu Ahl-us-Sunnah Yemen wanauawa na Hawthiyyah Raafidhwah. Wakati huo huo al-Qaa´idah ipo huko kwa silaha zake na nguvu zake za kijeshi. Hawakufanya hatua yoyote siku hata moja ili kuwalinda Ahl-us-Sunnah. Bali wanawacheka na wanafurahia hilo.

Je, tutarajie kheri yoyote kutoka kwa watu kama hawa? Wanaenda kinyume na wanachuoni. Ummah unaweza kupita katika mwelekeo wa sawa kwa kushikamana tu na wanachuoni. Kwa hivyo tusidanganyike kwa maneno ya kupambia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu wao:

“Wanazungumza vizuri na wanatenda vibaya.”

Hivi sasa wanasema kuwa wanataka kutangaza ukhaliyfah na kusimamisha Shari´ah ya Allaah, lakini kwa kutumia gharama za maisha ya Ahl-us-Sunnah. Wanataka kumuua kila anayeenda kinyume na wao. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba haijuzu kwa Muislamu kuwapenda. Haijuzu kwa Muislamu kuwaombea midhali hawaombei uongofu wao. Haijuzu kwa Muislamu, pasina kujali ni mahali gani alipo, kuwapa bay´ah.

Ninawanasihi kumhimidi Allaah kwa hali mliyomo. Bakieni katika miji yenu. Watiini viongozo wenu kwa yale yasiyokuwa kumuasi Allaah na wanasihiini kwa njia za Kishari´ah. Linganieni katika Tawhiyd na Sunnah. Kwa hayo mtakuwa katika kheri – Allaah (´Azza wa Jalla) Akitaka.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=146456
  • Imechapishwa: 09/04/2015