Haifai kumswalia Muhammad pekee katika Tashahhud ya mwisho

Swali: Je, inafaa katika Tashahhud ya mwisho mswaliji akatosheka na kusema:

اللهم صل على محمد

”Ee Allaah! Msifu Muhammad.”

pasi na kutaja mamkizi yaliyosalia ya Ibraahiym (الصلاة الإبراهيمية)?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza mamkizi ya Ibraahiym. Kama mswaliji yuko na nafasi ni lazima aisome yote kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Maswahabah zake kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (43)
  • Imechapishwa: 05/07/2024