Swali: Haifai kujenga majumba marefu?

Jibu: Hapana, sio katika hali zote, kwa msemo mwingine ni katika mambo yenye kuchukiza. Maswahabah walijenga na wakarefusha majengo. Hapana vibaya ikiwa kuna haja ya kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alieleza hivo kuhusu waarabu na kwamba baada ya wao kuwa wachungaji kondoo na kwenye majumba ya udongo wataanza kushindana kurefusha majumba, jambo ambalo ni alama ya kuielekea dunia na alama ya Qiyaamah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukataza jambo hilo, alitoa maelezo tu.

Swali: Kurefusha kwa kuzidisha?

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Haitakikani kufanya kitu kisichokuwa na haja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24287/ما-حكم-رفع-البنيان-والتطاول-فيه
  • Imechapishwa: 23/09/2024