Swali: Ipo Hadiyth ambayo hutumiwa na Jamaa´at-ut-Tabliygh:

“Atakayeswali zile mbili za baridi ataingia Peponi.”

Je, ni Swahiyh?

Jibu: Ni Swahiyh. Imepokelewa na al-Bukhaariy. Makusudio ya zile mbili za baridi ni Fajr na ´Aswr. Hadiyth hii sio ya ajabu. Inahusiana na fadhilah za matendo mema. Ni Hadiyth Swahiyh. Laiti Hadiyth za Jamaa´at-ut-Tabliygh inapokuja katika usahihi zingelikuwa kama hii. Nyingi katika Hadiyth zao hazikuthibiti. Kuhusu Hadiyth hii ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (955) Tarehe: 1411-01-29/1990-08-20
  • Imechapishwa: 10/10/2021