Hadiyth ya kugawanyika kwa Ummah


Swali: Hadiyth ya kugawanyika kwa Ummah, Ummah umekubaliana na usahihi wa Hadiyth hii na himidi zote ni za Allaah, lakini kuko ambao wanawekea mashaka usahihi wa Hadiyth hii. Vipi mtu huyu ataraddiwa?

Jibu: Hayazingatiwi maneno yake na wala hahitajii kupigwa Radd. Sisi tuko na maneno ya wanachuoni na mahufadhi juu ya kusahihisha Hadiyth hii na nguvu yake. Huyu anataka kuruhusu mfarakano. Huyu mwenye kuponda Hadiyth anataka mfarakano na anahimiza watu juu ya mfarakano na hataki Ummah uwe kitu kimoja. Mtu huyu ni katika walinganizi wa fitina.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5432
  • Imechapishwa: 06/09/2020