Hadiyth “Nilimuona mtu akitembea Peponi kwa sababu… “

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

127 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimuliakuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لَقدْ رَأيْتُ رَجُلًا يَتَقَلَّبُ في الجَنَّةِ في شَجَرَةٍ قَطَعَهَا مِنْ ظَهْرِ الطَرِيقِ كَانَتْ تُؤذِي المُسْلِمِينَ

“Nilimuona mtu akitembea Peponi kwa sababu ya mti alioukata njiani uliokuwa ukiwaudhi waislamu.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili inayoonyesha kuwa Pepo ipo hivi sasa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu huyu akitembea ndani yake. Hili ni jambo limefahamishwa na Qur-aan, Sunnah na wamekubaliana kwalo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wamesema kuwa Pepo ipo hivi sasa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[2]

Bi maana imetayarishwa. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa ipo hivi sasa. Hali kadhalika Moto upo hivi sasa. Havitotoweka. Allaah ameviumba ili viendelee kubaki. Vilevile yule atayeingia ndani ya Pepo au Moto hatoisha pia. Yule ambaye atakuwa ni katika watu wa Peponi atabaki humo hali ya kuwa ni mwenye kudumu milele. Yule ambaye atakuwa ni katika watu wa Motoni atabaki humo hali ya kuwa ni mwenye kudumu milele.

[1]Muslim (1914).

[2] 03:133

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/175)
  • Imechapishwa: 03/06/2024