Hadiyth kuhusu swalah ya Tasaabiyh ni dhaifu

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya Tasaabiyh na ni sababu zipi za kusihi kwake au kubatilika kwake ikiwa si sahihi?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana kuhusu Hadiyth za swalah ya Tasaabiyh. Maoni ya sawa ni kwamba swalah hiyo si sahihi na kwamba ni Hadiyth dhaifu na inayopingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh zilizo mashuhuri kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu swalah ya kujitolea, swalah ambayo Allaah amewachagulia waja Wake katika Rukuu´ zake, sujuud zake na mengineyo. Kwa sababu hiyo maoni ya sawa ni ya wale waliokwenda na msimamo wa kutosihi kwake. Ibn-ul-Jawziy (Rahimahu Allaah) ameitaja swalah hii katika ”al-Mawdhuu´aat”.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2256/ما-سبب-القول-ببطلان-صلاة-التسابيح
  • Imechapishwa: 08/01/2026