Imaam an-Nawawiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
190 – Abu Sa´iyd al-Kkhudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
(إيَّاكُمْ وَالجُلُوسَ في الطُّرُقَاتِ) فقالوا: يَا رَسُول الله، مَا لنا مِنْ مجالِسِنا بُدٌّ، نتحدث فِيهَا. فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (فَإذَا أبَيْتُمْ إلا المَجْلِسَ، فَأَعْطُوا الطَّريقَ حَقَّهُ). قالوا: وما حَقُّ الطَّريقِ يَا رسولَ الله؟ قَالَ: (غَضُّ البَصَرِ، وَكَفُّ الأَذَى، وَرَدُّ السَّلامِ، وَالأمْرُ بِالمَعْرُوفِ، والنَّهيُ عن المُنْكَرِ). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
“Ninawaonyo na kukaa kwenye njia.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hatuna budi isipokuwa kukaa tukizungumza.” Akasema Mtume wa Allaah: “Endapo hamna namna isipokuwa kukaa, basi ipeni njia haki yake.” Wakauliza: “Ni ipi haki ya njia, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kuinamisha macho, kuondosha maudhi, kurudisha salamu na kukataza maovu.”[1]
Ametaja mambo matano:
1 – Kuinamisha macho. Inamisheni macho kutomtazama mpitaji, ni mamoja ikiwa ni mwanaume au mwanamke. Mwanamke ni lazima mtu kuinamisha macho yake na asimtazame. Vivyo hivyo mwanaume inatakiwa kuinamisha macho usimtazame. Usimkodolei macho mpaka ujue ana nini.
Hapo mwanzoni mtu alikuwa akija na vitu vinavyohitajika nyumbani kila siku akivibeba mkononi na watu hawa wanamuona na kusema ana nini na kadhalika. Siku si mbali sana ilikuwa pindi anapopita mtu na yuko na nyama zake anaipelekea familia yake, basi watu wanaanza kumsema kuwa fulani leo ameiletea familia yake nyama na kadhalika. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema kuinamisha macho.
2 – Kuondosha maudhi ya kimaneno na kimatendo:
1 – Maudhi ya kimaneno ni kumsema mtu wakati anapopita au baada ya kuwa kishapita kwa kumsengenya na kueneza uvumi.
2 – Maudhi ya kimatendo ni kumbana mtu kwa kiasi cha kwamba ukakosa kumpa mwenzako nafasi mpaka akaudhika na akawa hawezi kupita isipokuwa kwa tabu na shida.
3 – Kurudisha salamu. Akikusalimia mtu mrudishie salamu. Hii ni moja miongoni mwa haki ya njia. Sunnah ni mpitaji kumsalimia aliyekaa. Ikishakuwa Sunnah ni namna hii anapokusalimia mrudishie salamu.
4 – Kuamrisha mema. Mema ni kila kile ambacho Allaah (Ta´ala) amekiamrisha au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi na wewe unatakiwa kukiamrisha. Ukiona mapungufu kwa yeyote, ni mamoja ikiwa ni katika wapitaji au wengine, basi mwamrisheni mwema. Badala yake msisitizeni yaliyo na kheri na kumpendezesha nayo.
5 – Mkiona mpitaji yeyote anafanya maovu, kwa mfano anapita na huku anavuta sigara au mfano wa hayo, basi mkatazeni. Hii ni haki ya njia.
Katika Hadiyth hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anawaonya waislamu kukaa kwenye njia. Ikiwa hana budi isipokuwa akae basi aipe njia haki yake.
[1]al-Bukhaariy (2465) na Muslim (2121).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (2/441-443)
- Imechapishwa: 24/08/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (2/441-443)
Imechapishwa: 24/08/2025
https://firqatunnajia.com/hadiyth-ipeni-njia-haki-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket