Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

206 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَنْ ظَلَمَ قيدَ شِبْرٍ مِنَ الأرْضِ، طُوِّقَهُ مِنْ سبْعِ أرَضينَ

“Atakayedhulumu ardhi kiasi na shibri basi [siku ya Qiyaamah] atabebeshwa ardhi saba.”[1]

Kudhulumu ardhi ni katika madhambi makubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kugeuza alamaza ardhi[2].  Mtu akigeuza alama ya ardhi kwa kuingiza sehemu ya jirani yake katika ardhi yake, basi mtu huyo amelaaniwa kupitia ulimi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maana ya laana kilugha ni mtu kuwekwa mbali na rehemaza Allaah. Vilevile amepewa adhabu nyingine iliyotajwa katika Hadiyth hii ya kwamba atabebeshwa siku ya Qiyaamah ardhi saba.

[1] al-Bukhaariy (2453) na Muslim (1612).

[2]Muslim (1978).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/496-497)
  • Imechapishwa: 02/09/2025