Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
05- Mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuzusha katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo, basi atarudishiwa mwenyewe.”
Kwa hivyo inatakiwa kwa mwanafunzi kuitilia umuhimu Hadiyth hii umuhimu mkubwa na aitumie kama hoja katika kila mahala pake stahiki kwa kuraddi Bid´ah na mambo ya uzushi katika maneno, matendo na mambo ya imani. Hakika ni asli katika mambo yote haya.
“… yale yasiyokuwemo…”
Kwa kuwa anaweza kuanzisha kitu kwa mujibu wa hali za watu, lakini uhakika wa mambo ni Sunnah iliyosuswa na watu. Hivyo atakuwa ameanzisha Sunnah iliyo kwenye dini na akawambusha nayo watu. Mtume (´alayhis-Salaam) amesema:
“Yule atakayeweka katika Uislamu msingi mzuri, basi ana ujira wake na ujira wa yule atakayeifanya pasina kupungua chochote katika ujira wake.”
“Mwenye kuzusha…”
Bi maana mambo ya uzushi katika dini. Dalili ya hilo ni kauli yake:
“… katika amri yetu hii…”
Bi maana dini yetu hii. Amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Shari´ah yake.
- Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 120
- Imechapishwa: 17/05/2020
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
05- Mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuzusha katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo, basi atarudishiwa mwenyewe.”
Kwa hivyo inatakiwa kwa mwanafunzi kuitilia umuhimu Hadiyth hii umuhimu mkubwa na aitumie kama hoja katika kila mahala pake stahiki kwa kuraddi Bid´ah na mambo ya uzushi katika maneno, matendo na mambo ya imani. Hakika ni asli katika mambo yote haya.
“… yale yasiyokuwemo…”
Kwa kuwa anaweza kuanzisha kitu kwa mujibu wa hali za watu, lakini uhakika wa mambo ni Sunnah iliyosuswa na watu. Hivyo atakuwa ameanzisha Sunnah iliyo kwenye dini na akawambusha nayo watu. Mtume (´alayhis-Salaam) amesema:
“Yule atakayeweka katika Uislamu msingi mzuri, basi ana ujira wake na ujira wa yule atakayeifanya pasina kupungua chochote katika ujira wake.”
“Mwenye kuzusha…”
Bi maana mambo ya uzushi katika dini. Dalili ya hilo ni kauli yake:
“… katika amri yetu hii…”
Bi maana dini yetu hii. Amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Shari´ah yake.
Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 120
Imechapishwa: 17/05/2020
https://firqatunnajia.com/hadiyth-ambayo-ni-hoja-dhidi-ya-bidah-zote/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)