Swali: Je, ule uchemba unaondoka nikiondoka na dereva wa kiume pamoja na watoto wadogo?

Jibu: Watoto hawasaidii kitu. Ni lazima awe pamoja nawe mwanaume asiyeweza kukuoa au mwanamke mwengine au mwanaume mwengine mwaminifu. Watoto hawasaidii kitu.

Swali: Hata kama wamefikisha miaka ya kubaleghe?

Jibu: Inapokuja katika umahram. Safarini au kuondosha uchemba. Kuondosha uchemba jambo lake ni jepesi na anaweza kuondosha uchemba asiyekuwa Mahram, hata hivyo akaondosha ule uchemba. Hata hivyo haifai kusafiri naye. Kusafiri ni khatari zaidi… hata hivyo ikiwa wakiwa na umri wa miaka kumi na nne na karibu na hapo, nyumbani wanasaidia [kuondosha ile faragha].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23924/هل-تنتفي-الخلوة-بوجود-الاطفال
  • Imechapishwa: 01/06/2024