Fanyeni kila kitu isipokuwa tendo la ndoa

Swali: Ikiwa mwanamke yuko katika hedhi na mume wake anataka kustarehe naye, lakini yeye anaogopa kuwa kustarehe huko kunaweza kupelekea lililokatazwa na hivyo anajiepusha naye katika kipindi hicho. Je, anahesabiwa kuwa ni mwanamke muasi?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Fanyeni kila kitu isipokuwa tendo la ndoa.”[1]

Kwa maana kwa mwanamke mwenye hedhi. Kwa hiyo inajuzu kwa mume kustarehe naye kwa kulala pamoja na kumbusu bila ya kumwingilia. Ikiwa mwanamke anajua kuwa mume wake anafanya uzembe na anaweza kuvuka mipaka, basi hakuna ubaya kwake kujiepusha naye ili asije akaangukia katika kosa kubwa lililokatazwa, khaswa ikiwa anamjua kwa kulegea katika dini. Ama ikiwa anamjua kuwa ni mtu mwenye kujizuia na anayeshikamana na dini, basi hakuna ubaya kwake kumruhusu astarehe naye kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Fanyeni kila kitu isipokuwa jimaa.”[2]

[1] Muslim (455).

[2] Ibn Maajah (286).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mjamuu´-ul-Fataawaa (21/187)
  • Imechapishwa: 17/03/2026